Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 16 ambaye yuko kwenye mpango wa kutaka kuwa mtu mdogo kuliko wote kuendesha Ndege akiwa peke yake akizunguka dunia ametua salama Jijini Nairobi nchini Kenya. Marc Rutherford ambaye ni raia wa Uingereza na Ubelgiji aliianza safari yake nchini Bulgaria mwezi Machi.
–
“ilikuwa ngumu kidogo kuona mbele nilipokuwa napita kwenye jangwa la Sahara, lakini uzuri wa muonekano wa eneo lile kutokea juu ulifanya kila kitu kuwa rahisi.Kwa safari hii ninategemea kuwahamasisha vijana kufuata ndoto zao” alisema Marc baada ya kushuka kutoka kwenye ndege yake ndogo katika uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi.
–
Kampuni iliyotengeneza ndege hiyo Shark Aero ilikataa kushirikiana na Marc katika mpango wake. “Marc ni rubani mzuri sana hilo halina wasiwasi lakini safari hiyo ina hatari ambazo zinaweza kushindwa kukwepeka na kijana huyu bado ni mdogo.” Alisema msemaji wa kampuni hiyo.
–
Safari ya Marc itampeleka kwenye nchi nyingine 4 barani Afrika kabla hajaelekea Mashariki ya Kati, Asia, Amerika ya Kaskazini na baadae kurudi Ulaya. Marc ametokea kwenye familia ya marubani, baba yake pamoja na dada yake wote ni marubani.