Mashirika ya Ndege nchini Nigeria kuanzia Jumatatu ijayo yatasimamisha safari za Ndege za ndani ya nchi ili kupinga kupanda kwa bei ya Mafuta.
Bei ya mafuta ya ndege imepandishwa karibia mara 4 ndani ya mwaka huu kitu ambacho umoja wa mashirika ya ndege nchini humo umekiita kuwa sio kitu “rafiki kwa maendeleo”.
Wasafiri wote wa ndani ya nchi wanaopanga kusafiri kwa ndege wameombwa kutafuta njia mbadala za safari zao kuanzia Jumatatu.
Kupanda huko kwa bei ya mafuta kumesababishwa na uvamizi uliofanywa na Urusi nchini Ukraine.
Licha ya kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta katika bara la Afrika, Nigeria huagiza kutoka nje karibia mafuta yote ya ndege.