Kundi la muziki nchini Kenya Sauti Sol limetishia kushtaki kampeni za urais za Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kwa madai ya ukiukaji wa hakimiliki.
–
Akaunti za mitandao ya kijamii za Odinga zinasemekana kutumia wimbo wa Sauti Sol wa Extravaganza wakati wa kumtambulisha Martha Karua kama mgombea mwenza wa Muungano wa Azimio la Umoja.
ADVERTISEMENT
–
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter, Sauti Sol walilalamika kuhusu matumizi ya muziki wao katika kampeni zinazoendelea za kisiasa
ADVERTISEMENT