Baada ya CAF kuipiga Simba SC. faini ya $ 10000 (Tsh. milioni 23) kwa kuwasha moto katikati ya uwanja wa Orlando Pirates nchini South Africa kitendo ambacho kilihusishwa na imani za kishirikina, Msemaji wa Yanga Haji Manara ameandika haya;
–
“Wakati Watanzania tunaendelea kutangaza Filamu kubwa ya Royal Tour kuna wenzetu leo wamepigwa faini ya Dola Elfu kumi kwa kufanya Matambiko Hatarishi ugenini. Yaan Sisi tukitangaza Nchi yetu Kwa Vivutio vyake, Wenzetu wengine Kwa Maksudi wameenda kuiambia Dunia,,Sisi ni Wanga na Wachawi.
–
Nchi imefedheheshwa,, Watanzania Tumedhalilishwa na Mpira wetu tumeutia doa, kama Senior Citizen wa Taifa hili nimejisikia kinyaa kwa aibu hii kubwa zaidi kuwahi kutokea katika Taifa letu. ,,halaf huo Ulozi wenu mliufanya ndani ya Mwezi wa Ramadhani,,Daaah sijui nife tu,,maana aibu hii haivumiliki kwa kweli.
–
Ipo haja ya Watanzania kuombwa Radhi kwa hii fedheha tuliyoipata leo, Vinginevyo wanapaswa pia kupewa adhabu ya ndani ikiwemo kufungiwa miaka kumi kuwakilisha Nchi..
–
lazma Tanzania ichukue hatua sahihi za ndani ili aibu hii isirudie tena, Kesho nasafiri kwenda Ulaya itabidi nihairishe,,maana huko Airport za wenzetu nikitoa Passport tu, watajua na mimi Mwanga. Yaan Mnaenda kuwanga huku Dunia inaona? Mnakwenda kuloga bila haya? Halaf wapo Wachambuzi walitaka eti tuwaige,, Tuige kuwanga? Tuige kukalia Moto? Tuige Shirki? Tuwaige kuroga?BARB. Shame On YouAAA”