ADVERTISEMENT
Msanii wa Filamu za Bongo na Mjasiriamali, Rose Alphonce maarufu kama ‘Muna Love’ amewalalamikia watu ambao kupitia mitandao ya kijamii wanamzushia kuwa amefariki dunia kitu ambacho hadi yeye kinamshangaza huku akisema kuwa yeye hatakufa bali ataishi kuutangaza ukuu wa Bwana na kama akimaliza basi ataenda kupumzika na si kufa kama wanavyo muombea.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Muna Love ameandika ; “Mimi sitakufa Bali nitaishi ili kutangaza ukuu wa Bwana nikimaliza kazi basi ntaenda kupumzika. Ila kwa sasa bado nipo sanaa tu mintakufa nikiwa mzee sana”.
–
“Na nyie mnaoniombea hili Mungu awabariki na kuwapa maisha marefu 😭😭 nimetumiwa sasahivi nimebaki Sina lakuwaambia ila Mungu atashughulika na nyinyi 😭🙏🙏🙏. Atakama unipendi ndo uniuwe nikiwa hai ? 🥲🙏 Izo YouTube ni sehemu za kuumiza wenzenu?🥲”
ADVERTISEMENT