Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itakwenda Benin kwa ndege maalumu kwa ajili ya mechi ya Kundi F ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Niger itakayochezwa Juni 4 jijini Cotonou Benin.
–
Niger ambao ndiyo wenyeji wamechagua kuchezea mechi zao jijini Cotonou kutokana na uwanja wao kutopitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kutokidhi vigezo.
ADVERTISEMENT