ADVERTISEMENT
Licha ya kupoteza mchezo wake wa nyumbani wa kuwania kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Burundi, timu ya Taifa ya wanawake U17 (Serengeti Girls) wamefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2.
–
Mchezo wa awali Serengeti Girls waliibuka wababe ugenini kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Burundi. Goli la mchezaji wa Burundi Bora Ineza la dakika ya 83 limeipatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Serengeti Girls ya Tanzania katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
–
Katika kipindi cha kwanza Estella Gakima wa Burundi Aliifungia timu hiyo bao la kuongoza kabla ya Rehema Mohamed wa Tanzania kusawazisha.
–
Kwa matokeo hayo Tanzania imefanikiwa kusonga mbele na sasa inatarajiwa kucheza na mshindi wa mchezo baina ya Zambia ama Cameron mwishoni mwa mwezi Mei.
ADVERTISEMENT