Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa taarifa kuwa imeona mjadala wa malalamiko kutoka kwa Wadau Mtandaoni kuhusu watoa huduma kubadili bei za vifurushi kimyakimya na kusema kuwa inafuatilia suala hilo kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli.
–
“TCRA ingependa kuwajulisha kuwa endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi kupitia 0800008272.
–
“Pia unaweza kuwasiliana na Mamlaka kupitia baruapepe dawatilahuduma@tcra.go.tz. Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli” taarifa ya TCRA.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT