Mshambuliaji wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, 29, anapanga wa kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu mustakabali wake baada ya mwekezaji Mmarekani Todd Boehly kukamilisha ununuzi wa klabu hiyo wa thamani ya £4.25bn.
–
Mabingwa wa Ligi kuu ya England Manchester City wanamfuatilia beki wa Leicester City wa wa chini ya miaka 18, Ben Nelson, mwenye miaka 18.
–
Real Madrid wameendelea kuweka juhudi zao za kumnunua kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 22, kwa dau la takriban £68m.
–
Winga wa zamani wa Chelsea na Arsenal Willian, 33, anatamani kuondoka nchini kwao Brazil, ambako kwa sasa anachezea Corinthians, na kurejea kucheza soka Ulaya.
–
Nottingham Forest wana nia ya kumbakiza kwa mkopo beki wa Middlesbrough Djed Spence lakini Tottenham, Arsenal na Brentford pia wanamfuatilia Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 21.
–
West Ham wako tayari kumuuza beki Mfaransa Issa Diop, 25, ambaye kwa sasa amekuwa chaguo la nne chini ya mkufunzi David Moyes.
–
Mshambuliaji wa Benfica, Darwin Nunez, 22, amekuwa akikutana na baadhi ya timu kubwa za ligi kuu England kuhusu uwezekano wa kuhama katika majira haya ya joto. Liverpool, Manchester United na Newcastle zote zinavutiwa na raia huyo wa Uruguay.
–
Manchester United wameanza mazungumzo ya kumsajili beki wa kimataifa wa Uholanzi, Jurrien Timber, 20, anayechezea Ajax ambaye thamani yake ni pauni milioni 43.
–
Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30, hajaiambia mpaka sasa Liverpool kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo huku kukiwa na tetesi za kutaka kuhamia kwa mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich kwa pauni milioni 35.