ADVERTISEMENT
Manchester City wiki ijayo ihuenda ikatangaza usajili wake ghali wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 2. (Sun)
–
Liverpool inaongoza mbio zinazozijumuisha pia klabu za Real Madrid na Chelsea katika kuwania saini ya kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni, 22. (Marca via Metro)
–
Arsenal inaweza kugonga mwamba katika mpango wake wa kumsajili mshambuliaji Lautaro Martinez, 24 ambapo Inter Milan inaonekana haitamuuza. (Gazetta Dello Sport)
–
Arsenal, Chelsea na Manchester United zinamuwania kiungo wa RB Leipzig Christopher Nkunku, 24, msimu huu. (Football.London)
–
Bayern Munich inaandaa ofa ya kwanza ya £15m ili kuanza mazungumzo na RB Leipzig kwa ajili ya kiungo wake Konrad Laimer. (Fabrizio Romano on Twitter)
–
Hata hivyo, Manchester United pia inamtaka nyota huyo mwenye miaka 25 ambaye awali aliwahi kufundishwa na mkufunzi wa sasa wa muda wa United Ralf Rangnick. (Mirror)
–
Kiungo wa zamani wa Manchester United David Beckham ana matumaini mshambuliaji Cristiano Ronaldo, 37, atasalia Old Trafford msimu ujao. (Talksport)
–
Kiungo wa zamani Fred Rutten amefichua kwamba amekataa ofa ya kuwa mmoja wa wasaidizi wa Erik ten Hag, Manchester United akijiandaa kurudi PSV Eindhoven. (Guardian)
–
Tottenham Hotspur itakabiliana na upinzani kutoka klabu za Bundesliga na Serie A kwa ajili ya kiungo wa Hellas Verona kutoka Czech Antonin Barak, 27. (Inside Futbal)
–
Liverpool wanamatumaini ya kuipiku Leeds katika usajili wa £4m wa mlinzi wa Aberdeen Calvin Ramsay,19. Kinda huyo anaandaliwa kumsaidia Trent Alexander-Arnold. (Goal)
–
Meneja wa zamani wa Chelsea na Spurs Andre Villas-Boas anaweza kuwa kocha wa Morocco, na kufungua milango ya kurejea kwa Hakim Ziyech kwenye timu ya taifa. (Le360 via Sun)
ADVERTISEMENT