ADVERTISEMENT
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa kurudisha fomu za maombi ya leseni za Klabu msimu wa 2022/2023 kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship na First League mpaka Mei 10, 2022.
–
Timu itakayorudisha fomu katika muda huo italazimika kulipa faini shilingi 500,000 kabla ya Mei 6 na shilingi 1,000,000 kuanzia Mei 7-10, 2022.
–
Mwisho wa zoezi la kurudisha fomu bila faini ilikuwa Aprili 25, 2022.
–
Fomu zinarudishwa Makao Makuu ya TFF, Karume, Ilala kwenye Ofisi ya Meneja wa Leseni za Klabu.
ADVERTISEMENT