ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, March 22, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

TFS KANDA YA KUSINI KUTUMIA FILAMU YA ROYAL TOUR KUONGEZA WATALII KUSINI

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 15, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
TFS KANDA YA KUSINI KUTUMIA FILAMU YA ROYAL TOUR KUONGEZA WATALII KUSINI

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

0
SHARES
143
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

Mar 21, 2023

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

Mar 21, 2023

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

Mar 21, 2023
Load More

Na Muhidin Amri,
Masasi

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Kanda ya Kusini, imejipanga kutumia Filamu ya Royal Tour  kuendeleza na kutangaza  vivutio mbalimbali   vinavyopatikana katika misitu inayosimamiwa na TFS kwa lengo ka kuvutia watalii na kuleta ajira kwa vijana wa kanda ya Kusini.

Hayo yamesemwa na Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Bi Manyise Mpokigwa wakati akizungumzia  walivyojipanga  namna watakavyotumia  Filamu hiyo iliyozinduliwa wiki iliyopita na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuongeza mapato ya nchi kupitia sekta ya misitu.

Alisema,Filamu ya Royal Tour imekuja kwa muda muafaka kwani TFS  itahakikisha inatumia fursa hiyo kutangaza vivutio na maliasili  zinazopatikana katika misitu inayosimamiwa na wakala Kanda ya Kusini kwa ajili ya kuvutia watalii wa ndani na nje ambao watalipa fedha kwa ajili ya kutembelea na kuangalia vivutio na maliasili zilizopo Kanda ya Kusini.

Aidha Kamishina Mpokigwa, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza Tanzania Kimataifa na imani ya Watanzania Filamu hiyo itaongeza watalii wengi na wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya utalii.

Mpokigwa ambaye ni Kamanda wa  wakala wa Huduma za misitu(TFS)Kanda ya Kusini alisema, Kanda ya Kusini kuna vivutio vingi,hata hivyo bado havijafahamika sana kutokana na changamoto mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kamanda Mpokigwa,TFS kanda ya Kusini ina misitu mitatu ya asili mojawapo ni Msitu wa Londo uliopo katika mkoa wa Lindi,ambako kuna maeneo mazuri ya kupumzika na Mti maarufu wa Nyerere  wenye Historia kubwa.

Alisema,mti huo umekuwa kivutio kikubwa tangu ulipogundulika hasa baada ya Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Nyerere alipofika na kuchuna gamba  la mti huo na kuondoka nalo.

Alisema,kuanzia wakati huo jamii na watu  kutoka maeneo mbalimbali wanaendelea kutumia magamba ya mti huo kama tiba na kufanya matambiko ambayo kwa imani zao wanafanikiwa kutokana na shida zinazowakabili.

“sasa mti huo kupitia wakala wa huduma za misitu umewekewa utaratibu maalum ambao kila  anayefika katika eneo hilo kwa ajili ya kuchuna magamba analazimika kuchangia kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kuchangia mapato ya nchi yetu”alisema.

Mpokigwa,alitaja kivutio kingine ni msitu wa Pindilo uliopo katika wilaya ya Kilwa ambao ni  sehemu nzuri kutokana na uwepo uoto wa asili unoafaa kwa ajili ya watu kupumzika.

Pia alisema,katika msitu huo kuna mto Nyange na Bwawa lenye Wanyama aina ya Boko ambao ni walemavu wa ngozi(Albino)wenye uwezo wa kuongea na mtu na ni kivutia kikubwa kwa watu wanaofika katika msituo huo.

Kwa mujibu wa Mpokigwa,katika mkoa wa Ruvuma kuna safu za Milima  maarufu ya Matogoro Manispaa ya Songea wenye aina mbalimbali za ndege na ndiyo chanzo cha mto maarufu wa Ruvuma unaotenganisha kati ya Tanzania na Nchi jirani ya Msumbiji.

Alisema, katika milima  hiyo kuna maeneo mazuri yanayofaa kwa ajili ya kufanya mikutano mbalimbali  kwa kuwa ni sehemu nzuri na tulivu ikilinganisha na maeneo mengine ya  katika mkoa huo.

Alitaja Msitu  mwingine ni Mwombesi(Mwombesi Nature Reserve) unaopatikana katika wilaya ya Tunduru wenye Wanyama wengi mchanganyiko kama vile Tembo,Nyati, Swala,Paka pori, Fisi,Nyoka na maporomokoya asili.

Alisema,Msitu wa Mwombesi  ni hifadhi iliyo mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Msumbuji kupitia Mto Ruvuma na mwaka 2021 watalii zaidi ya 50 kutoka Mataifa mbalimbali walitembelea katika msituo huo na kufanya mkutano.

Alisema,kwa sasa kazi kubwa inayofanyika ni kuboresha mazingira hasa ya miundombinu ya barabara ili Watanzania na watalii kutoka nje ya nchi waweze kufika katika msituo huo.
MWISHO.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI
HABARI

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA
HABARI

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI
HABARI

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
BIKIRA JANE APATA MTOTO
HABARI

BIKIRA JANE APATA MTOTO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA
HABARI

ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO
HABARI

SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In