Ameandika msemaji wa Simba, Ahmed Ally;
“Wengi tumeumizwa na matokeo ya jana sio kwa sababu tumepata sare lakini kuna ubora hatukuuona kwenye timu yetu. Poleni wana Lunyasi πhamstahili haya mnayopitia, lakini kuna wakati unalazimika kuyapokea kwa sababu ndo gharama za kupenda mpira.
Hatuwezi kujificha kwenye kivuli cha kwamba timu yetu itafanya vizuri milele, lazima tukubali ya kwamba kuna panda shuka lazima tupitie. Na wakati mwingine ni muhimu kuyafurahia makosa yako ili ujue wapi uboreshe
Kadri inavyonyesha ndipo tunaona panapovuja na hii itatusaidia kuwa bora nyakati zijazo
Maumivu tunayopitia sisi mashabiki na wachezaji wetu wanapitia hayohayo kwani hakuna anaependa kuharibu kazi yake. Kwa sasa tuendelee kusimama imara ili tumalize msimu na TAJI MOJA kati ya MATAJI MAWILI makubwa hapa nchini
Lengo ilikua ni kuchukua mataji yote mawili lakini sasa TUTAGAWANA, Insha Allahπ hatuwezi kumaliza msimu patupu”