Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtinika amesema kutokana na utamaduni uliojengeka suala la hedhi limekuwa halizungumziki mara kwa mara katika jamii na kufanya uelewa wa jambo hilo kutofahamika kwa mapana yake.
–
Pia amesema Wadau mbalimbali wa hedhi wanapokutana na kukumbuka kundi la wasichana na kutoa elimu inasaidia kuongeza uelewa ambalo ni kawaida kwa mwanamke.
–
Mtinika amezungumza hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi taulo za Kike kwa wasichana wenye ulemavu wa shule ya msingi Jeshi la Wokovu, ambapo amesema ni changamoto katika shule nchini juu ya usalama wa watoto hasa wakike wanapokuwa katika siku zao za hedhi.
–
Kwa Upande wake Mratibu wa Taasisi ya Care 4 disability , Penina Malundo amesema kundi la watoto wa kike wenye ulemavu mara nyingi linasahaulika katika jamii, hivyo wameona vyema kuungana kwa kuchangisha fedha kwa watu binafsi pamoja na mashirika katika kusaidia kundi hilo.
–
Amesema taasisi hiyo imeweza kukusanya takribani taulo za kike 300 na kugawa katika shule hiyo pamoja na shule ya msingi Mtoni maalum.