Msanii na Staa wa Pop kutoka Nchini Marekani Britney spears na mpenzi wake Sam Asghari wamedhibitisha kuharibika kwa ujauzito wa mtoto wao.
–
kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram Britney Ameandika..
“Kwa huzuni mkubwa tunalazimika kutangaza kwamba tumempoteza mtoto wetu mapema katika ujauzito, Huu ni wakati wa huzuni kwa mzazi yeyote, Labda tulitangaza mapema sana kuwa tunategemea kupata mtoto,hata hivyo tulifurahi sana kuwapa habari njema muda huo, Upendo wetu kwa kila mmoja ndio nguvu yetu, Tutaendelea kujaribu kupanua familia yetu nzuri.”