Urusi imesitisha usambazaji wake wa gesi asilia kwa Finland, kampuni ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Finland ya Gasum imesema.
–
Finland imekuwa ikikataa kulipa vifaa vyake kwa sarafu ya Urusi rubles lakini pia ni kufuatia taarifa za Finland kuwa itaomba uanachama wa NATO.
–
Kampuni ya Gasum imesema hatua hiyo ni ya kusikitisha lakini ikasema hakutakuwa na usumbufu kwa Wateja, licha ya mzozo wa Ukraine, Urusi inaendelea kusambaza gesi kwa nchi nyingi za Ulaya.
–
Baada ya mataifa ya Magharibi kuiwekea vikwazo Urusi kutokana na vita hivyo, Urusi ilisema nchi zisizo rafiki lazima zilipe gesi kwa kutumia sarafu ya Urusi, hatua ambayo Umoja wa ulaya ilichukualia kama kulazimisha kwa kutoa vitisho, kutegemea nishati ya Urusi ni sababu inayochangia katika kupanda kwa gharama za maisha kunakowakabili Watumiaji wengi.