ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, March 20, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Vodacom Tanzania Yazindua Huduma ya Bima ya Afya kupitia mfumo wa M-Pesa

I am Krantz by I am Krantz
May 14, 2022
in HABARI
0
Vodacom Tanzania Yazindua Huduma ya Bima ya Afya kupitia mfumo wa M-Pesa
0
SHARES
250
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Mkurugenzi wa Mpesa , Epimack Mbeteni akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima “Linda afya na VodaBima” uliofanyika jijini Dar es salaam, Vodacom kwa kushirikiana  na kampuni za Jubilee Insurance ,Mo Assurance pamoja na Milvik Tanzania watatoa huduma za bima ya afya inayolenga  kutumia  mfumo wa kidijitali katika utoaji wa huduma za afya jumuishi nchini

RelatedPosts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

Mar 20, 2023

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

Mar 20, 2023

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

Mar 20, 2023
Load More

Meneja Masoko wa M-Pesa, Noel Mazoya akizungumza kabla ya uzinduzi wa huduma ya VodaBima “Linda afya na VodaBima”  kwenye ofisi za makao makuu ya Vodacom jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa M-pesa , Epimack Mbeteni (wa pili kulia) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Insurance, Dinpankar Acharya (kushoto), Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia Malalamiko (TIRA), Okoka Mgavilenzi (watatu kulia), Afisa  Bima Mkuu Mo Assurance, Pamela Ndosi (wa pili kushoto),  mkuu wa Kitengo cha Mauzo Milvik, Ismail Simanga (Watatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja ya uzinduzi rasmi wa huduma ya  VodaBima “Linda afya na VodaBima”

 

Huduma hiyo mpya chini ya VodaBima ni kwa ushirikiano na Jubilee Insurance, Mo Assurance na Milvik Tanzania.

 

13 Mei 2022, Vodacom Tanzania Plc, kampuni inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano, nchini leo imetangaza ushirikiano na Milvik kutoa huduma za bima ya afya kutoka Jubilee Insurance na Mo Assurance inayolenga  kutumia dijitali katika utoaji wa huduma za afya jumuishi.

Upanuzi huu unakuja baada ya kampuni hiyo kufanikiwa kwa bidhaa zake za bima ya magari kupitia VodaBima ambayo inatoa huduma za bima kubwa na ndogo kwa ushirikiano na kampuni 10 zinazotoa huduma za bima wanaoongoza nchini, jambo ambalo litawezesha Watanzania kupata huduma muhimu za afya.

ADVERTISEMENT

Vifurushi vya bima ya Afya kutoka kwa washirika hawa vitaweza kuwafikia kwa urahisi wateja na vinapatikana kwenye huduma za Vodacom M-Pesa. Vifurushi hivyo ni vya bei nafuu na vinatarajiwa kurahisisha mchakato wa matibabu ya afya nchini. Vifurushi vilivyoanzishwa ni pamoja na malipo wagonjwa wanaolazwa hospitalini, ajali, maisha na bidhaa iliyounganishwa (Faraja Yangu) ambayo hutoa faida na kwa wengine, kwa kuwahusisha watu wazima na watoto na hutofautiana kwa bei kulingana na umri wao na virufushi maalum.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa, Epimack Mbeteni    alisema, “Tuna furaha kubwa leo kuweza kutangaza maendeleo haya muhimu katika utoaji wa bima kwa Watanzania. Vodacom Tanzania imeweka mkazo mkubwa kwenye afya kama kichocheo kikuu cha shughuli zetu zinazoongozwa na malengo. Huduma ya afya ni hitaji la msingi kwa Watanzania wote na tunaamini inapaswa kupatikana kwa urahisi kwa wote, hivyo ushirikiano wetu na Milvik, Jubilee na Mo assurance utasaidia kufungua hitaji hili.”

Vodacom imekuwa ikishiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma za afya nchini kwa miaka mingi, imeweza kutoa msaada katika maeneo tofauti kama vile matibabu ya fistula ya uzazi, msaada na matibabu kwa watoto wachanga na familia zao. Mwezi uliopita, kampuni pia ilifanikiwa kuzindua mpango wake wa m-mama kusaidia wanawake wajawazito wanaopata dharura wakati wa kujifungua.

ADVERTISEMENT

Vifurushi hivi vya bima ya afya vinakuja kufuatia mapokezi chanya ya bima ya magari iliyoanzishwa mapema mwaka huu kwa ushirikiano na kampuni 10 za bima ambapo sasa Watanzania watafurahia urahisi wa kununua bima kutoka eneo lolote nchini bila adha ya kutembelea ofisi za wakala yeyote wa bima.

Vodacom Tanzania PLC inaendelea kufanya kazi ya kutoa suluhu za kibunifu zaidi kwa wateja wake, juhudi ambazo hivi karibuni zimeiwezesha kupata tuzo ya mtoa huduma bora ya mtandao wa simu kutoka Tume ya TEHAMA nchini.

Kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Meneja Utekelezaji Sheria na kushughulikia malalamiko (TIRA), Okoka Mgavilenzi alisema serikali inahimiza matumizi ya teknolojia katika kupata na kutoa huduma muhimu za kidijitali ikiwemo bima. “Tunaipongeza Vodacom Tanzania kwa kuja na ubunifu huu na kuchukua hatua kubwa ya kuongeza watoa huduma wengi wa bima kwenye mtandao wa kidijitali wa VodaBima ambao tunaamini utaongeza kwa kasi kikubwa upatikanaji na matumizi ya huduma ya bima nchini hasa katika eneo la afya ambayo umezindua leo,” alisema Mgavilenzi.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Milvik, Ismail Simanga alisema tukio hilo lilikuwa hatua kubwa sana ambayo itashuhudia afya ya famiia ikilindwa vyema na bima bora ya afya. “Afya na usalama wa famila yako inamaanisha ulimwengu kwako. Tunaelewa na tunataka kukusaidia kuwalinda wapendwa wako dhidi ya hali zilizo nje ya uwezo wako”.

Kupitia jukwaa la MPesa watanzania wataweza kupata bima zetu popote pale walipo bila tabu yoyote.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO
HABARI

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”
HABARI

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA
HABARI

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO
HABARI

TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR
HABARI

WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI
HABARI

MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In