Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ametangaza kutowafukuza Bungeni wabunge 19 wa viti maalum kutokea CHADEMA baada ya kukosa sifa kwa mujibu wa sheria.
–
Spika amesema wataendelea kutumia nafasi hiyo ya viti maalum hadi shauri lao la kufukuzwa uanachama litakapoamuriwa na Mahakama Kuu.
ADVERTISEMENT
–
“Nilipokea barua za wabunge hao 19 (Halima Mdee na wenzake 18) wakinijulisha uamuzi wa kuwavua uanachama wakisema si halali na kinyume cha Katiba ya Tanzania na hawakupewa nafasi ya kujitetea na wabunge hao wamepinga uamuzi huo Mahakama Kuu ya Tanzania” Spika Dkt. Tulia Ackson
ADVERTISEMENT