Wanafunzi 19 na waalimu wawili wamefariki dunia kwa kupigwa risasi baada ya mtu mmoja kufanya shambulizi katika shule ya msingi kusini mwa Texas nchini Marekani.
–
Maofisa wa usalama wamesema kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alifyatua risasi katika shule hiyo kabla ya kuuawa na polisi.
ADVERTISEMENT
–
Taarifa zinasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amejihami kwa bunduki yenye uwezo wa juu.
Kabla ya kufanya shambulizi hilo katika shule hiyo, kijana huyo anadaiwa kumpiga risasi bibi yake.
ADVERTISEMENT