Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameitaka wizara ya elimu kuharakisha mchakato wa kuwezesha Wanafunzi wa ngazi ya Diploma waingie kwenye Mpango Wa kupata Mkopo ili waweze kujikimu kama ilivyo wanafunzi wa ngazi ya digrii.
–
ADVERTISEMENT
Majaliwa ametoa kauli hiyo Jijini Arusha mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha Mei 24, 2022.
–
Waziri mkuu amesema Wanafunzi wa vyuo wanaomaliza ngazi ya diploma wamekuwa mhimili mkubwa kwenye ajira kwa kuwa wao ndio hutumika kwa kiwango kikubwa.
ADVERTISEMENT