Watanzania wameitwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia mapambano hayo. Mashindano yanatarajia kufungwa kesho majira ya saa 10 jioni.
–
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Yusuph Singo, amesema kuwa lengo ni kuunga mkono na kuwapa moyo mabondia hao waweze kufanya vizuri na kuona walivyojiandaa.
–
Amesema kuwa mashindano hayo yameshirikisha mabondia kutoa Zambia, Uganda na Tanzania . Akizungumzia viwango vyao amesema kuwa vipo vizuri na makocha watatumia kufanya maboresho. Wakati huo huo Shaibu Baruti mwenye uzito wa (Light Weight 60 Kg amempiga kwa pointi 3-0 mpinzani wake Djafari Nshmirimana huku Alex Isendi uzito wa (Light Welter 63.5 akiibuka na ushindi wa pointi 3-0 dhidi ya Mahataneeric wote kutoka Burundi.
–
Mwingine ni Bondia Elius Damson aliyeibuka na Ushindi pointi 2-0 dhidi ya mpinzani wake Rally Zrkoze naye kutoka Burundi waliopigana katika uzito wa (Welter Weight 67 Kg). Pambano la awali liliwakutanisha mabondia wa kike Magrethy Itembo kutoka Zambia aliyeibuka na pointi 3-0 dhidi ya Teddy Nakumul kutoka Uganda, huku Mwendo Mwale kutoka Zambia akitwaa pointi 3-0 dhidi ya bondia Kassim Ally kutoka magereza. Wengine ni bondia Andrew Chilata kutoka Zambia aliyeibuka na pointi 3-0 dhidi ya Shabani Mganda kutoka Jeshi la Kujenga Taifa.
–
Bondia Tukumuhebwa kutoka Uganda aliyeibuka na pointi 3-0 dhidi ya Joseph John kutoka Magereza, Mwande Shapt kutoka Zambia aliyemshinda kwa pointi 3-0 Shaban Hamadi wa Jeshi la Magereza. Kibira Owen kutoka Uganda aliyempiga kwa (KO) Sabura Fransis wa JKT uzito wa 67 kg huku uzito wa (71 Kg Light middle) Ziuba Stephan kutoka Zambia akimpiga kwa pointi 2-0 Kassim Mbudwike (Taifa), Yusuph Ally Magereza hakufika kwa bondia Senyange Zebra kutoka Uganda.
–
Wakati Joseph Philip bondia kutoka timu ya Jeshi la Magereza akifunga dimba kwa kumtwanga kwa pointi 3-0 bondia Nduwarugila Nestory kutoka Burundi. NA VICTORIA GODFREY