ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO
0
SHARES
214
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More

Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Bw.Abdallah Salum akiongea na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Halotel leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya inayojulikana kwa jina la “Toboa na Halotel 4G” inayowapa wateja wote wa Halotel walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Simu Kajanja Mpya kabisa ikiwemo iPhone 13 Promax maarufu kama “Macho Matatu” kila wiki. Mteja anapaswa kubadili laini yake ya 3G kuwa 4G au kusajili Laini mpya ya 4G na kutumia intaneti ili kuweza kupata fursa ya kuingia kwenye droo ya kuwa mshindi. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa Halotel.

 Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Masoko Ms. Sakina Makabu akitoa ufafanuzi wa Promosheni mpya, kwa waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Halotel leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Promosheni mpya inayojulikana kwa jina la “Toboa na Halotel 4G” inayowapa wateja wote wa Halotel walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Simu Kajanja Mpya kabisa ikiwemo iPhone 13 Promax maarufu kama “Macho Matatu” kila wiki. Mteja anapaswa kubadili laini yake ya 3G kuwa 4G au kusajili Laini mpya ya 4G na kutumia intaneti ili kuweza kupata fursa ya kuingia kwenye droo ya kuwa mshindi. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa Halotel. 

Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Bwa.Abdallah Salum na Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Masoko wakizindua rasmi Promosheni mpya inayojulikana kwa jina la “Toboa na Halotel 4G” inayowapa wateja wote wa Halotel walioko mjini na vijijini fursa ya kujishindia zawadi za Fedha Taslimu kila siku pamoja na Simu Kajanja Mpya kabisa ikiwemo iPhone 13 Promax maarufu kama “Macho Matatu” kila wiki. Mteja anapaswa kubadili laini yake ya 3G kuwa 4G au kusajili Laini mpya ya 4G na kutumia intaneti ili kuweza kupata fursa ya kuingia kwenye droo ya kuwa mshindi. Promeshini hii itaendeshwa kwa muda wa wiki nane (8) ni maalumu kwa wateja wa Halotel.

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Halotel Tanzania imeendelea kuwahakikishia wateja ubora na kasi ya mtandao wake kwa kuwapa huduma zenye ubunifu na kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano hapa nchini.

Wakati ikifanya jitihada hizo, Halotel pia imekuwa ikibuni bidhaa mpya zenye lengo la kuwazawadia wateja wake wanaotumia huduma za mtandao.

Mkurugenzi wa biashara cha Halotel, Bw. Abdallah Salum amesema: “Leo kampuni ina habari njema kwa wateja wetu: tunazindua kampeni mpya ya mtandao wa 4G. Kampeni hiyo inaitwa ‘Toboa na Halotel 4G.’

Kampeni hii itawapa fursa wateja kushiriki katika promosheni hii itakayoendeshwa kwa wiki 8 ambapo washindi watapata zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na simu janja.

Ili kushiriki katika promosheni hii ya Toboa na Halotel 4G, wateja ambao wanatumia 3G wanaweza kubadili laini kwenda 4G bila gharama yoyote au  mteja anaweza kusajili laini ya 4G na kuanza kutumia vifurushi vya intaneti kwa gharama nafuu na moja kwa moja atakuwa katika nafasi ya kuingia kwenye droo ya bahati na kuweza kuibuka mshindi.

Pia mteja anapaswa awe ameshatumia angalau 100MB ndani ya siku tatu kuanzia siku aliyoanza kutumia mtandao wa 4G. aliongeza Bw. Salum.

Kampuni itawazawadia washindi 10 kila siku, kila mmoja atapata fedha taslimu kiasi cha shilingi 100,000.

“Kila wiki washindi watatu (03) watazawadiwa simu janja ambapo mshindi wa kwanza atapata IPhone 13 pro max, mshindi wa pili atapata Samsung galaxy S22, na mshindi wa tatu atapata Samsung Galaxy A72,” Bw Salum alisema.

Kampuni imezindua kampeni hii kwa kuzingatia kwamba tayari mtandao wake wa 4G umeenea katika maeneo mengi ambapo kwa sasa ina vituo vipatavyo 1037 vinavyosambaza mtandao wa 4G, hivyo mtandao wa 4G umeongeza nguvu na ufikiaji wa maeneo mengi ya nchi.

Sababu zingine za kuanzisha kampeni hii ni kuwapa wateja uzoefu juu ya ubora wa 4G huku ikiwapitia zawadi mbalimbali, na hivyo kufanya huduma hiyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa sasa mtandao wa 4G umewafikia asilimia 45 ya Watanzania.    

“Hii ni kutokana na kukua kwa huduma za kidijitali hapa Tanzania na kuongezeka kwa uhitaji katika soko, na hivyo uwekezaji mkubwa wa kampuni umeelekezwa kwenye miundombinu katika juhudi za kuongeza vituo vya usambazaji mtandao wa 4G,” amesema Bw. Salum.

Ameongeza kuwa katika maeneo ambayo yana mtandao wa 2G kampuni itaboresha na kuwa 3G na maeneo yenye 3G watapata 4G.

Halotel itawekeza zaidi kuongeza ubora wa mtandao Kwa sababu Watanzania milioni 29.8, au karibu nusu ya Watanzania wanatumia huduma za intaneti, tafiti mpya inaonesha kuwa Halotel ina mtandao wenye kasi zaidi kuliko mitandao yote hapa nchini.

Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kampuni imekuwa ikijielekeza katika mikakati ya kupanua wigo wa mtandao wake hapa Tanzania.

Kwa kuzingatia kuwa asilimia 30 ya wateja wake wanatumia mtandao wa intaneti, kampuni inapanga kuongeza idadi hiyo kufikia asilimia 40 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Halotel tayari imeanza kuzindua kizazi cha nne cha huduma za mtandao wa 4G katika maeneo mengi ya nchi.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
TWITTER YATANGAZA KUONDOSHA BLUE TICK KUANZIA APRILI 1
BIASHARA

TWITTER YATANGAZA KUONDOSHA BLUE TICK KUANZIA APRILI 1

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In