ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

WATU 1.728 WABAINIKA KUWA NA KIFUA KIKUU WILAYANI TUNDURU

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 14, 2022
in HABARI
0
WATU 1.728 WABAINIKA KUWA NA KIFUA KIKUU WILAYANI TUNDURU

Bacteria which cause tuberculosis Mycobacterium tuberculosis, 3D illustration

0
SHARES
247
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Na Muhidin Amri,
Tunduru

RelatedPosts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023

Habari Kuu Kwenye Magazeti ya Leo Machi 28,2023

Mar 28, 2023

TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Mar 27, 2023

NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Mar 27, 2023
Load More

HOSPITALI ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma  imefanikiwa kuibua wagonjwa 1,728 wenye maambukizi ya kifua kikuu kuanzia mwaka 2020 hadi Mwezi Machi 2022.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt Wilfred Rwechungura, wakati akielezea mafanikio na mikakati ya kampeni ya kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu  inayoendelea katika wilaya hiyo.

Dkt Rwechungura alisema,kuanzia mwaka 2020 Hospitali ya wilaya  chini ya kitengo  hicho imekuwa  na mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa  wa TB kwani kila mwaka wanavuka malengo wanayopewa na Wizara ya Afya.

ADVERTISEMENT

Alisema,mwaka  2020 malengo ilikuwa kuibua wagonjwa 647, lakini  kutokana na mikakati  waliyojiwekea na kutekeleza waliibua wagonjwa 709 wanaume 387 na wanawake 322.

Aidha alisema kati ya watu hao walioibuliwa,watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na tano ni 221,na watoto 105 walio chini ya miaka mitano walipata dawa kinga(IPT) na 171 wanaoishi kwenye familia za wagonjwa wa TB ya mapafu walichunguzwa.

Dkt Rwengura aliongeza kuwa,katika kipindi hicho watu waliopimwa virusi vya ukimwi walikuwa 709 ambapo 79 waligundulika kuwa na  virusi vya ugonjwa huo na wote wameanzishiwa Dawa.

Kwa mujibu wa Dkt Rwechungura, mwaka 2021  malengo ilikuwa kuibua wagonjwa 741,hata hivyo walifanikiwa kuibua 768 kati yao wanaume 403 na wanawake 365  ambapo watoto walio chini ya miaka 15 walikuwa 289 huku waliopimwa VVU ni 768 na waliokutwa na maambukizi ni 55.

Alisema, mwaka huo  2021 familia za watoto walio chini ya miaka mitano  wenye TB ya mapafu ambao walichunguzwa ni 221 na walioanzishiwa dawa kinga walikuwa 179 na watu 13 walipoteza maisha.

Pia alieleza,kwa mwaka 2022 wamepewa malengo ya kuibua wagonjwa 841,lakini katika kipindi cha robo ya tatu mwaka iliyoanzia Mwezi Januari hadi Machi,tayari wamefanikiwa kuibua jumla ya watu 251 kati yao wanaume 139 na wanawake 112.

Dkt Rwechungura alisema,katika muda huo watoto  walio chini ya umri wa miaka 15 waliogundulika kuwa na TB ni 77 na waliopima VVU walikuwa 251 ambapo  watu 9  wamekutwa na maambukizi na wote wameanzishiwa Dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo .

Naye Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya hiyo Dkt Mkasange Kihongole alisema, katika miaka mitatu tangu kuanza kwa kampeni  kabambe ya uelimishaji na uibuaji wa ugonjwa huo kumekuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Alisema,mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mkubwa wa watumishi wa idara ya afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi wa Hospitali ya wilaya na wahudumu ngazi ya jamii(CHW).

Alisema, wahudumu ngazi ya jamii wamekuwa msaada mkubwa katika kampeni hizo kwa kuwa wanaokwenda kwenye mikusanyiko ya watu ikiwamo shule za bweni na maeneo mengine kwa ajili ya kutoa elimu ya kifua kikuu na kuchukua sampuli za makohozi na kupeleka Hospitali kwa ajili ya vipimo.

Mkasange alisema,katika malengo ya mwaka huu Hospitali ya wilaya imepewa lengo la kuibua wagonjwa 200,Hospitali ya Misheni Mbesa 150,Hospitali ya Kiuma 100,vituo vinavyopima makohozi Matemanga wagonjwa 15,Nakapanya 15,Mkasale 15,Mtina 15,Mchoteka 15 Zahanati ya Nandembo 10 na Namiungo  wagonjwa 10.

Aidha,amewashukuru wadau Shirika la MDH-Amref Heath Africa kwa mchango mkubwa  wanaotoa wa kuwapa mafunzo wahudumu ngazi ya jamii na watumishi wa afya ambayo yamesaidia sana kuongeza morali ya utendaji na uwajibikaji kwa watumishi wa sekta ya afya.

Kwa mujibu wa Dkt Mkasange,ugonjwa wa TB unatibika kwa mtu aliyeambukizwa na mwenye dalili  za ugonjwa huo kufika Hospitali kwa ajili ya uchunguzi na anayebainika anaanzishiwa matibabu.

ADVERTISEMENT

Ameitaka jamii kuacha mila potofu zinazohusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina na amelipongeza Gazeti la Habarileo kwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu.

Mkazi wa Tunduru aliyewahi kuugua ugonjwa wa kifua kikuu na kupoma Salome Golihama,ameishukuru serikali kuhamasisha jamii kujitokeza kwenye kampeni na elimu ya kifua kikuu kwa wananchi.

Alisema,hatua hiyo imesaidia sana jamii kufahamu dalili za ugonjwa huo na kujitokeza kwa hiari  kupima na kuanza matumizi ya dawa ambazo zinatolewa bure.
MWISHO.

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Habari Kuu Kwenye Magazeti ya Leo Machi 28,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION  KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
HABARI

TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

by Ally Hamis Zingizi
Mar 27, 2023
NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
HABARI

NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

by I am Krantz
Mar 27, 2023
Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo
HABARI

Naibu Waziri aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya michezo

by I am Krantz
Mar 27, 2023
MZEE WA MIAKA 92 AFUNGA NDOA YA TANO MWAKA MMOJA BAADA YA NDOA NNE KUVUNJIKA
HABARI

MZEE WA MIAKA 92 AFUNGA NDOA YA TANO MWAKA MMOJA BAADA YA NDOA NNE KUVUNJIKA

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023
BAKWATA YASHIKILIA MSIMAMO NDOA MIAKA 14
HABARI

BAKWATA YASHIKILIA MSIMAMO NDOA MIAKA 14

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In