Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaodaiwa kuchoma moto gari la Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyamilanda wilayani humo, Emmanuel Sheiza nyumbani kwake.
–
Nguvila alitoa agizo hilo alipotembelea eneo la tukio na baadaye kuongea na wanakijiji wa kitongoji cha Nyamilanda na kuelezea masikitiko yake.
–
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Mei 9, 2022 ambapo watu wasiofahamika walichoma moto gari la Hakimu huyo ambaye anaishi kwenye nyumba za Mahakama zilizopo jirani na Mahakama ya Mwanzo Nyamilanda.