Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewataka wachimbaji wadogo nchini kutumia fursa zinazowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kutafuta wafanyabiashara na kampuni kubwa ili kushirikiana katika kukuza uwekezaji kwenye sekta madini.
ADVERTISEMENT
–
Wito huo ameutoa mkoani Mwanza wakati akihitimisha ziara yake kwenye mgodi wa Busolwa Mining uliopo wilayani Misungwi ulioanzishwa kwa ushirikiano wa kikundi cha wananchi cha Isinka na mwekezaji, pamoja na mambo mengine Waziri Biteko amewahikikishia Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ili wawekeze na kukuza mitaji yao.
–
‘’Unajua suala la kuitwa mchimbaji mdogo kila siku siyo sawa ni lazima ifike mahali mvuke hapo ,Serikali imewapa fursa nyingi sana ni lazima wapambane kutoka kwenye uchimbaji mdogo kwenda wa kati,nafahamu yapo matatizo mengi kwenye sekta ya madini lakini Rais ametuwekea mfumo mzuri kuanzia kwenye maeneo ya uchimbaji, masoko ya kuuzia madini na kuondoa urasimu ambao ungewachelewesha watu kuchimba madini.
ADVERTISEMENT