ADVERTISEMENT
Mtandao wa Entertainment Tonight imethibitisha kuwa mwigizaji mashuhuri duniani Will Smith amekuwa akipata msaada na matibabu ya jinsi ya kumudu Hasira na hisia zake baada ya tukio la kumpiga kofi Mchekeshaji Chris Rock kwenye tuzo za Oscar March 27, 2022.
–
Hii inatajwa kuwa hatua ya kwanza ya Will Smith kujaribu kuonyesha watu kuwa amebadilika na anaweza kuendelea na kazi zake za kutengeneza filamu.
–
Kama ulipitwa, Will Smith alimchapa Kofi Chris Rock baada ya mchekeshaji huyo kutoa utani uliomkosesha raha mke wa Will Smith, Jada Pinkett Smith.
ADVERTISEMENT