Wizara wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum imeliomba Bunge kujadili na kuidhinisha jumla ya Shilingi 43,403,061,000 ili kutekeleza majukumu yake kwa maendeleo na ustawi wa jamii.
–
Akizungumza leo Bungeni waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, Dkt.Dorothy Gwajima (Mb) wakati akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/2023 amesema katika mwaka 2022/23, Wizara inakadiria kutumia kiasi cha Shilingi 32,310,981,000 kwa ajili ya Matumizi 104 ya Kawaida.
–
Kati ya fedha hizo, Shilingi 18,169,057,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi 14,141,924,000 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi.
–
na katika upande wa shughuli za maendeleo, Dkt.Gwajima amesema Wizara inakadiria kutumia Shilingi 11,092,080,000 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 6,900,000,000 ni Fedha za Ndani na Shilingi 4,192,080,000 ni Fedha za Nje.