Wakati taarifa zikidai mshambuliaji kinara wa mabao ndani ya klabu ya Yanga yuko mbioni kutimkia Kaizer Chiefs klabu zote mbili zimekanusha taarifa juu ya dili hilo.
–
Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema hakuna kitu kama hicho juu ya Mayele kuondoka.
–
“Mayele haondoki Yanga, tutakuwa nae msimu ujao. Kuna waandishi wawili wa Ghana ndio wanatuvuruga na nitawajibu. Fiston akiondoka Yanga mimi pia NITAONDOKA nitakuja hapo redioni kuaga.” Senzo Mbatha
–
Naye mtoto wa mmiliki wa klabu ya Kaizer Chiefs Kaizer, Motaung Junior amekanusha taarifa hizo kupitia akaunti yake ya Twitter akiandika kwa kifupi “msimu wa habari za kipuuzi unaendelea”.