Kampuni ya uwekezaji kutoka Marekani, RedBird Capital imekubali kuinunua klabu ya AC Milan kwa Euro 1.2bilioni kutoka kwa kampuni ya usimamizi wa uwekezaji ya Amerika, Hedge fund Elliott.
–
Milan ni moja ya klabu ambayo ilikuwa inamilikuwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi.
–
RedBird, tayari wameshafanya uwekezaji katika Fenway Sports Group, kampuni abayo inamiliki klabu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu ya England na klabu ya baseball, Red Sox pia wanamiliki hisa kwenye klabu ya Toulouse ambayo iko nchini Ufaransa.