Mwanaume aliyejaribu kumuua Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan ameachiwa huru miaka 41 baadae. Mnamo mwaka 1981 John Hinckley Jr ( 67) alimjeruhi vibaya Rais Reagan kwa kumpiga risasi.
–
Hinckley alikaa kwa miaka mingi katika kitengo cha watu wenye matatizo ya akili jijini Washington baada ya kuachiliwa huru kwa tatizo la kichaa kwenye kesi yake mwaka 1982.
ADVERTISEMENT
–
Hivi sasa mwanaume huyo ameachiwa huru kabisa na hatohitaji tena usimamizi wa wataalamu wa sheria na magonjwa ya akili. Hinckley ameposti katika mtandao wa Twitter kuwa ” baada ya miaka 41 miezi 2 na siku 15, hatimaye uhuru!”.
ADVERTISEMENT