Klabu ya Azam FC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior kwa mkataba wa miaka miaka mitatu.
–
Nyota huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, amesajiliwa na Azam FC akitokea timu ya Sol FC ya kwao, Kipre Junior alikuwepo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.
Kiungo huyo mshambuliaji, 22, mwenye kipaji cha hali ya juu pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.
–
Ubora wake ulimfanya pia kuchezea timu za Taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) 2020.