Na Emmanuel Madata Lubigisa, Shabiki wa Azam FC
–
Ni wakati wa kufanya kazi kwa kufata misingi na taratibu za kazi, Kwanza naomba nianze kwa kuwapongeza wamiliki, viongozi, walimu na wachezaji wote wa @azamfcofficial kwa kila mmoja kuwajibika katika majukumu yake, mpaka kufika hapa tulipo ni nguvu zenu na sapoti yetu mashabiki wa @azamfcfansforum na mashabiki wengine, wote wapenda soka.
–
Kuna mambo kwetu mashabiki tunayatazama kama ni unyanyasaji wa kimtazamo kutoka kwa viongozi wetu kutotutendea haki katika baadhi ya maeneo katika timu yetu, eneo kubwa na la kwanza ni UONGOZI kutokuwa na scouting nzuri yenye kuleta wachezaji wa viwango vizuri na ushindani katika timu, hii ni kutokana na kusajiri kwa mazoea kama ambavyo ilikuwa ni kawaida kwa washindani wetu wa timu za K/KOO, hapo nyuma kugombea mchezaji wakati kuna mahali tulifika kama @azamfcofficial hizi timu zilihitaji zaidi wachezaji wetu kuliko sisi kuhitaji wachezaji wao zaidi, swali kujiuliza niwapi tuna feli,
–
Jibu ni rahisi VIONGOZI wameingia kwenye korongo la mto K/koo na tayari wamemezwa na sasa tunaishi humo. Eneo jingine ni wachezaji wenyewe kutojitoa kwa timu na kucheza ki mihemko na sio kutafuta ushindi kwa juhudi maarifa mbinu na kujitoa, timu yetu ni kubwa nje kwa kuitazama ila ndogo kwa uwajibikaji kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye quality zinazolingana, hii inaondoa upambanaji sambamba na VIONGOZI kutotoa motisha kwa wachezaji na kuishi kwa kutegemea mishahara pekee, haitoshi hata sisi wafanyakazi katika maeneo yetu ya kazi kuna marupurupu, tukiishi kwa mshahara pekee tutafanya kazi kwa mazoea na ndicho kinachotokea kwa wachezaji wetu
–
Hebu VIONGOZI tunapoelekea mkae kuona ni jinsi gani Maeneo muhimu yanafanyiwa kazi, WAMILIKI niwaombe mumuangalie POPAT kwa jicho la ndani ni mtu muhimu, lakini muda wa yeye kuwa alipo kwa sasa na soka letu linapoelekea hastahili kuwa hapo amefanya makubwa ila tunaomba kwa mapenzi yenu kama itawapendeza mumuondoe yeye na jopo lake, Mtuletee mtu/watu wenye taaluma zao na si wenye ujamaa na familia yenu.
–
MWALIMU apewe wigo mpana wa yeye kufanya maamuzi na machaguo ya wachezaji anaowahitaji ili kwendana na mifumo yake @ahamidmoallin anafaa kwa mitazamo yake, tatizo aina ya wachezaji aliokutana nao na ndio sababu ya yeye kila kukicha kuja na machaguo mapya kiwanjani katika kikosi chake, tatizo ni quality ya homa za vipindi kwa wachezaji wetu waliopo sambamba na majeruhi, kitu pekee ambacho namuunga mkono ni kupenda zaidi vijana kuliko wakongwe na hii ndio Falsafa yetu, Na ilipotea baada ya lile korongo kupitia wachezaji wetu tuliowalea kwa lengo la kupunguza bajeti lakini haikuwa tulivyodhani ikawa ni kuongeza bajeti kwa kuleta wachezaji wakuja kukaa bench na kuchukua hela za bure sambamba nakusitisha mikataba ya walimu, tunaowaongeza mikataba bila kuitumikia,
–
Tunatakiwa kuwa na malengo yetu kama timu sio MTU mmoja mmoja FALSAFA ya timu yetu imepoteza, falsafa yake ambayo tuliipenda tangu mwanzo na kuingia kwenye falsafa zisizo zetu, hapo awali tulicheza mpira mzuri na wa kuvutia inafika mahali unafungwa unaona ni matokeo ya mpira tofauti na sasa hii inatokana kuhama kwenye malengo ya awali, hapo mwanzo tuliwaaminu vijana wetu na kuwapandisha tofauti na sasa tulileta professional wenye uwezo mkubwa na waliwapa motivation vijana tofauti na sasa UPIGAJI NA CHUKI Timu yetu imekuwa korongo la kuwatengenezea mazingira wengine kufanikiwa hili ni janga na tiba yake ni moja tu.
POPAT OUT NA MSULULU WAKE