ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki Ya CRDB Kuendelea Kutoa Elimu Ya Fedha Kupitia Promosheni Ya Mzigo Flexi

I am Krantz by I am Krantz
Jun 7, 2022
in BIASHARA
0
Benki Ya CRDB Kuendelea Kutoa Elimu Ya Fedha Kupitia Promosheni Ya Mzigo Flexi
0
SHARES
132
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More
ADVERTISEMENT

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili akiongea na waandishi habari (hawapo pichani) kuhusu dhamira ya Benki hiyo kuendelea kutoa elimu ya fedha kupitia promosheni ya Mzigo Flexi ambapo Benki ya CRDB inalenga kuwafikia Watanzania katika vitongoji vyote vya Jiji laDar es salaam na Tanzania kwa ujumla ili kutoa elimu ya mpango maalum wa kuweka akiba ambao utawawezesha kupata riba ya hadi asilimia 9. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Badru Idd na Meneja wa Tawi la Azikiwe, Hamis Saleh.
=====  =====  =====
Benki ya CRDB imejipanga kuendelea kutoa elimu ya fedha kupitia promosheni ya Mzigo Flexi ambapo inalenga kuwafikia Watanzania katika vitongoji vyote vya Jiji la Daes salaam na Tanzania kwa ujumla, lengo likiwa kutoa Elimu ya mpango maalum wa kuweka akiba ambao utawawezesha kupata riba ya hadi asilimia 9.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika viunga vya Tawi la CRDB Benki lililopo Mtaa wa  Azikiwe jijini Dar es salam Mapema leo, Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili alisema; “Sisi kama Benki tumeamua kuwafikia Watanzania na kuwapa elimu ya fedha ili kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo ya muda mfupi, kati na mrefu”.
“Sambamba na kuwapa elimu lakini pia kupitia mpango huu Benki inatoa riba ya hadi asilimia 9 ili kutoa hamasa ya kuweka akiba ambapo kupitia promosheni ya Mzigo Flexi, mteja anaweza kuweka amana kwa muda wa kati ya miezi 3, 6, 12 au 24,” alisema Adili.
Promosheni ya ‘Mzigo Flexi’ inalenga watu binafsi, vikundi, taasisi na wafanyabiashara na mteja anaweza kuwa na mpango wa akiba wa ‘Mzigo Flexi’ zaidi ya mmoja na kuwekeza kwenye mikataba mingi. Kila mkataba utakuwa ni mkataba huru na bidhaa haina ada yoyote na riba inalipwa kwa akaunti ya kibinafsi ya mteja kulingana na kipindi cha riba kilichokubaliwa (Kila mwezi, Robo mwaka, Nusu mwaka, Kila mwaka au wakati wa kukomaa).
Iwapo mteja ataamua kughairi utaratibu wa ‘Mzigo Flexi’, atalazimika kupoteza asilimia 50 ya riba aliyopata na kuendelea kuweka fedha chini ya utaratibu mwingine wa kawaida wa benki.
Wateja wanaweza kupata mpango wa akiba wa “Mzigo Flexi” huo kupitia tawi lolote la Benki ya CRDB nchi nzima lakini pia anaweza kupata fomu ya maombi kupitia tovuti ya Benki na kuwasilisha katika tawi lolote la Benki ya CRDB baada ya kuzijaza.

 

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

TWITTER YATANGAZA KUONDOSHA BLUE TICK KUANZIA APRILI 1
BIASHARA

TWITTER YATANGAZA KUONDOSHA BLUE TICK KUANZIA APRILI 1

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
TCB YATOA MSAADA WA MABATI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI BUTIAMA
BIASHARA

TCB YATOA MSAADA WA MABATI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI BUTIAMA

by Ally Hamis Zingizi
Mar 22, 2023
MPYA: TigoPesa yazindua Kadi Mtandao (Tigo Pesa Mastercard)
BIASHARA

MPYA: TigoPesa yazindua Kadi Mtandao (Tigo Pesa Mastercard)

by ALFRED MTEWELE
Mar 22, 2023
BRELA YAWATAKA VIJANA KUSAJILI BIASHARA ZAO
BIASHARA

BRELA YAWATAKA VIJANA KUSAJILI BIASHARA ZAO

by ALFRED MTEWELE
Mar 14, 2023
USINUNUE GESI KWA WASIO NA MIZANI
BIASHARA

USINUNUE GESI KWA WASIO NA MIZANI

by ALFRED MTEWELE
Mar 9, 2023
BENKI YA AKIBA WAZINDUA WARIDI AKAUNTI   KWA  WANAWAKE WAJASIRIAMALI
BIASHARA

BENKI YA AKIBA WAZINDUA WARIDI AKAUNTI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

by I am Krantz
Mar 9, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In