ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, July 2, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Benki ya NMB Yakabidhi Bilioni 30.7 Gawio kwa Serikali

I am Krantz by I am Krantz
Jun 15, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
Benki ya NMB Yakabidhi Bilioni 30.7 Gawio kwa Serikali
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

 

RelatedPosts

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

Jul 2, 2022

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JULAI 2, 2022

Jul 2, 2022

Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.

Jul 2, 2022
Load More

 

 

 

 

ADVERTISEMENT

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (wapili toka kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 30.7 kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna (watatu toka kulia) ikiwa ni gawio kwa Serikali katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma leo. Wengine ni Waziri wa Fedha na Mipango ,Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba(wa pili kulia), Afisa Mkuu wa Fedha NMB(kushoto), Juma Kimori na wapili toka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.

 

Benki ya NMB leo wamekabidhi Sh. Bilioni 30.7 kwa Serikali huku Makamu wa Rais, Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango akisema benki hiyo imefanya siku yake na Serikali nzima kuwa yenye furaha.

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo kufuatia agizo lake kwa benki hiyo mwaka jana kipindi kama hiki alipopokea gawio la Sh Bilioni 20.8 ikiwa ni faida ya 2020 na kutaka waongeze nguvu na ubunifu ili waje na gawio nono.

Gawio hilo limetolewa ikiwa ni faida ya NMB kwa mwaka wa fedha ulioishia 2021 ambapo jumla ya Sh. Bilioni 97 zilipitishwa na mkutano mkuu wa wana hisa wa Benki ya NMB kutolewa kwa wanahisa kama gawio. Serikali ikiwa inamiliki hisa 31.8%, imepokea shilingi Bilioni 30.7 kama gawio lake kutoka benki ya NMB ikiwa ni ongezeko la 40% ukilinganisha na mwaka jana.

Kwa gawio hilo, Benki ya NMB ndani ya kipindi cha miaka mitano inakua imetoa jumla ya Sh. Bilioni 80.544 kwa Serikali.

 

Akipokea mfano wa hundi ya kiasi hicho, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango alisema benki hiyo imeendelea kuiheshimisha Serikali kwa kuonyesha namna gani inavyokuwa kimtaji na kuwajali wateja wake.

“Hata nitakapokwenda kumpokea Mheshimiwa Rais, hili litakuwa ni jambo la kwanza kumuambia, moyo wangu umeburudika sana, mmenifurahisha sana nasema hongereni sana,” alisema Dkt. Mpango.

 

ADVERTISEMENT

Akitoa taarifa yake kwa Makamu wa Rais, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema faida ya Benki baada ya kodi katika kipindi cha 2021 iliongezeka kwa asilimia 41 hadi kufikia Sh. Bilioni 290.

Kiasi hicho ni kikubwa ukilinganisha na Sh. Bilioni 206 ya mwaka 2020 ambapo idadi ya akaunti za wateja iliongezeka hadi kufikia Milioni tano ikilinganishwa na milioni nne za 2020.

“Katika kuhakikisha Benki inaendelea kuwa na maendeleo endelevu, tumeweza kuongeza mtaji wa Benki hadi Sh. Trilioni 1.3 na iliendelea kuwa na ufanisi, na kuweka rekodi ya uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato, kufikia asilimia 46,” alisema Zaipuna.

Zaipuna alisema kwa mwaka 2021, Benki ilipata Tuzo saba za kimataifa, ikiwemo ya benki bora nchini kwa mwaka wa tisa mfululizo ambayo iliyotolewa na Jarida la Kimataifa la Euromoney. Kwa mujibu wa Mtendaji huyo, hadi mwishoni mwa 2021, jumla ya mikopo ya Sh. Trilioni 4.3 ilikuwa imetolewa kwa wakulima, wafanyabiashara wadogowadogo, wa Kati na watu binafsi.

Akizungumzia mafanikio ya benki, alisema yalitokana na uwekezaji katika mifumo ya kidijitali, huduma za wakala, ambazo ziliongezeka na kufikia mawakala 10,194 ukilinganisha na 8,410 waliokuwepo 2020.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya NMB, Dkt. Edwin Mhede alisema gawio kwa mwaka wa 2022 wanatarajia kuwa na gawio nono zaidi kwani kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wamepata faida kubwa inayolingana na faida ya mwaka mzima katika kipindi cha miaka ya nyuma kutokana na ubunifu uliofanywa na watumishi wa benki.

Mwisho……


 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI
HABARI

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

by Shabani Rapwi
Jul 2, 2022
NEYMAR KUONDOKA PSG
HABARI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JULAI 2, 2022

by Shabani Rapwi
Jul 2, 2022
Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.
BIASHARA

Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.

by I am Krantz
Jul 2, 2022
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASA KWENYE NYAYA ZA UMEME
HABARI

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASA KWENYE NYAYA ZA UMEME

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022
MTUMISHI WA TANESCO AKUTWA GUEST AMEFARIKI
HABARI

MTUMISHI WA TANESCO AKUTWA GUEST AMEFARIKI

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022
SIKUKUU YA EID EL-ADH’HAA JULAI 10, 2022
HABARI

SIKUKUU YA EID EL-ADH’HAA JULAI 10, 2022

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In