ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Thursday, June 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

BENKI YA NMB YAKUBALIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR KUSIMAMIA UTUNZAJI WA BUSTANI YA FORODHANI

I am Krantz by I am Krantz
Jun 23, 2022
in HABARI
0
BENKI YA NMB YAKUBALIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR KUSIMAMIA UTUNZAJI WA BUSTANI YA FORODHANI
0
SHARES
201
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mkuu wa Biashara ya kadi NMB, Philbert Casmir akiongea kwenye mkutano huo kwenye hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar leo.

 

Mkuu wa wilaya ya Mjini Unguja, Rashid Simai Msaraka (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya NMB baada ya mazungumzo na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar.

 

 Benki ya NMB imefikia makubaliano na Serikali ya Zanzibar kutunza bustani ya Forodhani visiwani Zanzibar ikiwa ni moja ya juhudi zake za kuunga mkono azma ya uhifadhi wa mazingira visiwani humo na ajenda ya uchumi wa bluu.

Mradi huo wa utunzaji wa bustani ya Forodhani unalenga kuboresha mazingira ya kitalii na kuakisi vyema sifa maarufu ya eneo hilo, na utawezesha bustani hiyo kuvutia wageni wengi zaidi kila mwaka huku ukichangia kuchochea sekta ya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar jana wakati wa kutangaza Mashindano ya Mbio za Boti Zanzibar yanayodhaminiwa na Benki ya NMB na kutarajiwa kufanyika Jumamosi hii.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe. Rashid Simai Msaraka alisema benki hiyo imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo wa serikali ya Zanzibar na imekuwa mstari wa mbele kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo visiwani humo.

Alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi imekuwa ikiweka kipaumbele cha kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi na kuzitaka kampuni nyingi kuunga mkono mipango ya maendeleo ya serikali.

“Tumefanya kazi kwa karibu sana na Benki ya NMB katika miaka ya nyuma na nimedhihirisha na kutangaza kuwa tayari tumefikia makubaliano nao ya kuendeleza na kutunza bustani za Forodhani hapa Zanzibar,” Msaraka alisema.

Alibainisha kuwa pamoja na kuboresha mandhari ya eneo hilo, mradi huo utaleta manufaa makubwa na kusema, wakandarasi wazawa watazingatiwa huku akionyesha matumaini kuwa mradi huo utasaidia kuboresha sura ya Zanzibar.

RelatedPosts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 1, 2023

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 1, 2023

Jun 1, 2023

MAYELE;- TUNAENDA KUSHINDA KWAO USM ALGER

May 31, 2023

CCM YAZINDUA KADI ZA KIELEKRONIKI KUTUMIKA KAMA ATM

May 31, 2023
Load More

Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi wa NMB, Philbert Casmir wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo katika kusaidia ushirikishwaji wa fedha na kuongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa bidhaa zinazokidhi matakwa ya wateja.

Alisema mipango ya benki hiyo ni kuendelea kupeleka huduma karibu na wateja huku akiongeza kuwa benki hiyo ina mpango wa kupeleka huduma kwenye maeneo ya Wete, Nungwi, Mkoani, Uwanja wa ndege miongoni mwa maeneo mengine visiwani humo.

ADVERTISEMENT

Aidha, alisema kama sehemu ya dhamira ya benki yake kusaidia ushirikishwaji wa kifedha, Jumamosi hii itazindua Kampeni ya ‘Teleza Kidigitali’ visiwani humo inayotoa huduma za kibenki bila mafadhaiko na suluhu mbalimbali za kibenki za kielektroniki.

“Baada ya uzinduzi wenye mafanikio wa kampeni yetu ya ‘Teleza Kidigitali’ katika mikoa mingi nchini Tanzania, sasa ni zamu ya Zanzibar. Tumejipanga vizuri na kila kitu kipo tayari kwa uzinduzi wa Zanzibar Jumamosi hii hivyo watu wa Zanzibar wajiandae kupata uzoefu wa kipekee wa huduma za kibenki za kisasa,” alisema.

Katika hatua nyingine, Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Britam Insurance wamedhamini mbio za boti za Zanzibar za mwaka huu.

Kampuni hizo mbili zitatoa zawadi kwa washindi zinazofikia shilingi milioni sita na laki tano na zitatoa kifurushi cha bima ya ajali kwa washiriki wote kwa kipindi cha mwaka mmoja.

 

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 1, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 1, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
CCM YAZINDUA KADI ZA KIELEKRONIKI KUTUMIKA KAMA ATM
HABARI

CCM YAZINDUA KADI ZA KIELEKRONIKI KUTUMIKA KAMA ATM

by ALFRED MTEWELE
May 31, 2023
MKE WA RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI ASUMBULIWA NA KUPOTEZA KUMBUKUMBU
HABARI

MKE WA RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI ASUMBULIWA NA KUPOTEZA KUMBUKUMBU

by ALFRED MTEWELE
May 31, 2023
YALIYOJIRI KWENYE KURASA ZA MAGAZETI LEO MEI 21, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO MEI 31, 2023

by ALFRED MTEWELE
May 31, 2023
WHO YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAPAMBANO DHIDI YA MAGONJWA YA MLIPUKO
HABARI

WHO YAIPONGEZA TANZANIA KWA MAPAMBANO DHIDI YA MAGONJWA YA MLIPUKO

by ALFRED MTEWELE
May 31, 2023
TADB yashiriki maonesho ya wiki ya Maziwa  mkoani Tabora
HABARI

TADB yashiriki maonesho ya wiki ya Maziwa mkoani Tabora

by I am Krantz
May 30, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In