Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini Kimemfukuza rasmi Uwanachama Mwanasiasa MKongwe na aliekuwa Kada wa Chama hicho Mzee Baraka Mohamed Shamte Kutokana na Madai ya Kukashifu Madaraka ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.
–
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Katibu Mwenezi Mkoa wa Mjini Maulid Issa amesema kuwa kutokana na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Mjini chini ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Talib Ali Talib kimefanya Maamuzi ya kumuondoa Baraka Mohamed Shamte ndani ya Chama hicho.
–
“Tumefanya Maamuzi ya kumuondoa Kabisa Ndugu Baraka Mohamed Shamte na Kwa sababu ya kufanya vitendo vya kukashifu hadharani Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Dkt Hussein Ali Mwinyi,” Alisema.