KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, ametoa onyo kwa wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama wanaotumia majina ya viongozi wakuu kwamba wamewatuma kugombea.
–
Amesema viongozi hao wasibebeshwe wagombea kabla ya muda huku akikemea makatibu wa chama na Jumuiya za CCM ambao wameanza kubebwa na wagombea mifukoni na kuzungushwa kwenye hoteli.
–
Kiongozi huyo alitoa onyo hilo jana alipofungua kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kilichofanyika jijini hapo.
–
“Ni aibu unapokuta mtu mzima anatumia jina la kiongozi wake kwamba ‘huyu ndiye amenituma, huyu amenipa fursa, huyu ndio ameniambia nijiandae kuchukua fomu kugombea nafasi’.