ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, August 13, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

CRDB, USAID Na DFC Kutoa Shilingi Bilioni 100 Kwenye Sekta Ya Elimu, Afya, Biashara Ndogo Na Kati Pamoja Na Sekta Zisizo Rasmi Tanzania

I am Krantz by I am Krantz
Jun 30, 2022
in HABARI, MICHEZO
0
CRDB, USAID Na DFC Kutoa Shilingi Bilioni 100 Kwenye Sekta Ya Elimu, Afya, Biashara Ndogo Na Kati Pamoja Na Sekta Zisizo Rasmi Tanzania
0
SHARES
48
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) kwa pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wakionyesha hati za makubaliano ya mikopo ya uwezeshaji yenye thamani ya Bilioni 100 kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC kwa ajili ya kuiwezesha Benki hiyo kukopesha sekta mbalimbali nchini zikiwemo Sekta ya Ujasiriamali, kwa maana ya wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs), Sekta ya Elimu, Sekta ya Afya na biashara zisizo rasmi, muda mfupi baada ya kuzisaini katika hafla fupi iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. Picha zote na Othman Michuzi.

RelatedPosts

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

Aug 13, 2022

Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022

Aug 12, 2022

BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji

Aug 12, 2022
Load More

======  =====   =====

Dar es Salaam, Juni 30 2022 Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald J. Wright amethibitisha nia ya Serikali ya Marekani katika kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia ushirikiano mpya uliosainiwa katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC.

Kupitia ushirikiano huo, Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC yatashirikiana na Benki ya CRDB kuwezesha mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 100 za kItanzania. Ushirikiano huo utaiwezesha Benki ya CRDB kutanua wigo wa uwezeshaji wa mikopo wa wanawake na vijana sambamba na kutoa mikopo zaidi katika sekta za elimu, afya na sekta zisizo rasmi Tanzania nzima.

 “Benki ya CRDB inayo furaha kubwa kufanya kazi na USAID na DFC katika kusaidia biashara ndogo nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wakisaini hati ya makubaliano ya mikopo ya uwezeshaji yenye thamani ya Bilioni 100 kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC kwa ajili ya kuiwezesha Benki hiyo kukopesha sekta mbalimbali nchini zikiwemo Sekta ya Ujasiriamali, kwa maana ya wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs), Sekta ya Elimu, Sekta ya Afya na biashara zisizo rasmi. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.

ADVERTISEMENT

Biashara hizi ndogo na za kati ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania na tunaamini ushirikiano huu sio tu utasaidia kutanua wigo wetu wa kukopesha lakini pia kuwawezesha wafanyabiashara kwa kuwashauri na kuhakikisha wanafanya biashara kisasa kwa kutumia teknolojia. Lakini kubwa zaidi katika ushirikiano huu ni nia yetu ya kuwapa motisha wafanyabiashara wanawake na vijana katika safari yao ya ujasiriamali,” alisema Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

“Serikali ya Marekani inatambua kuwa hakuna chombo peke kinachoweza kutatua changamoto za Tanzania hivyo tunafurahi na kusheherekea mikataba hii miwili na Benki ya CRDB ambayo itaongeza ushirikishwaji wa kifedha na uwezeshaji kwa makundi muhimu kama vile wanawake na vijana,” alisema        Dkt. Donald J. Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wakisaini hati ya makubaliano ya mikopo ya uwezeshaji yenye thamani ya Bilioni 100 kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC kwa ajili ya kuiwezesha Benki hiyo kukopesha sekta mbalimbali nchini zikiwemo Sekta ya Ujasiriamali, kwa maana ya wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs), Sekta ya Elimu, Sekta ya Afya na biashara zisizo rasmi. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.

Ushirikiano huu unalenga kuboresha maeneo yafutayo;

-Mikopo katika Sekta ya Afya:      Benki itatoa mikopo ya hadi Shilingi Bilioni 20.3 katika sekta ya afya. Mikopo hii itatumika kusaidia katika ujenzi wa mahospitali, vituo vya afya, kliniki, vituo cha uchunguzi wa afya, maduka ya madawa na huduma za uzazi pamoja na ununuzi wa vifaa ya matibabu na ujenzi au ukarabati wa maeneo ya kutolea huduma za afya.

ADVERTISEMENT

-Mikopo katika Sekta ya Elimu:      Benki itatoa mikopo ya hadi Shilingi Bilioni 37.5 katika sekta ya elimu kusaidia katika mnyororo wa thamani wa elimu ikiwemo uanzishwaji wa elimu isiyolenga kupata faida, shule za msingi na sekondari zinazolenga misingi ya imani ya dini ambazo zitahudumia sekta ya elimU sambamba na utoaji mikopo kwa biashara zinazolenga kutoa upatikanaji wa vifaa vya elimu.

-Mikopo kwa Biashara Ndogo na Kati:  Benki itatoa hadi Shilingi Bilioni 17.9 katika sekta ya biashara ndogo na kati. Benki itajikita katika biashara za sekta zote za uchumi kusaidia katika mitaji ya uendeshaji, manunuzi ya vifaa, ujenzi na ubadilishwaji wa sehemu za biashara ili kukuza biashara.

-Mikopo kwa Sekta zisizo Rasmi: Benki itatoa hadi Shilingi Bilioni 23.1 kusaidia biashara zisizo rasmi kutoka katika sekta zote za uchumi ambapo kipaumbele kitakua kwenye biashara zinazoendeshwa na vijana na wanawake.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene
BIASHARA

Mkazi wa Mufindi -Iringa akabidhiwa gari mpya Suzuki S Presso baada ya kuibuka mshindi promosheni ya Vodacom Tusua Mapene

by I am Krantz
Aug 13, 2022
Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022
HABARI

Rais Samia Akiwa katika Ziara yake Mkoani Iringa 2022

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji
HABARI

BIL.11 kupelekwa Mafinga kuboresha miundombinu ya Mji

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Dkt. Mpango Aitaka NEMC na STAMICO Kufanya Tathimini Migodini
HABARI

Dkt. Mpango Aitaka NEMC na STAMICO Kufanya Tathimini Migodini

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Yanga yaagana na Afisa Habari wao, Hassan Bumbuli
MICHEZO

Yanga yaagana na Afisa Habari wao, Hassan Bumbuli

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 12.08.2022
MICHEZO

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 12.08.2022

by ALFRED MTEWELE
Aug 12, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In