MKUU wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri amepiga marufuku baadhi ya wafugaji wanaotumia vibaya silaha kwa kuwatisha na kuwapiga wafugaji.
–
Msafiri ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Wilaya ametoa maagizo hayo kwenye Kijiji Cha Kitomondo Kata ya Ruvu na kupata taarifa juu ya baadhi ya wafugaji wavamizi wanaotishia na kuwapiga wakulima kwa silaha mbalimbali na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
–
Amesema wafugaji hao wamekuwa na matumizi mabaya ya silaha mbali mbali zikiwemo bunduki na zile za jadi kama mishale na upinde na kutaka kukomeshwa kwa tabia hiyo na endapo kutatokea tukio la aina hiyo kamati hiyo haitosita kukomesha matumizi ya silaha hizo. Amesema kibali cha kumiliki silaha hakiruhusu raia kutishia raia mwingine silaha hivyo waaanza kutafakari umiliki wa silaha kwa watu wa aina hiyo.
–
Aidha amepiga marufuku mifugo kusambaza kiholela na kuagiza Serikali ya kijiji cha Kitomondo kukutana na wafugaji wiki ijayo ili kubaini wafugaji wavamizi na idadi ya wafugaji wanaotambuliwa kuomba kibali halali kwenye mkutano wa Kijiji. Nao wakulima wa Kitomondo ,Kidawa Omary na Hamza Botea Wamesema ,kumezuka wimbi la mifugo na wafugaji wavamizi Hali inayosababisha kuliwa mazao Yao na kupata hasara.
–
Naye Ofisa mifugo kata ya Ruvu Francis Ekoni amepokea maagizo hayo na kusema wafugaji wanaotambulika katika kijiji cha Kitomondo ni wanne tu. Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Kibaha Ombeni Msangi ameeleza kuwa, kuingiza mifugo eneo jingine, Kijiji kingine kwa wakulima ni kosa.