Nyota wa Mtibwa raia wa Kongo, Deo Kanda hatimae amepata leseni ya kuanza kuitumikia Mtibwa Sugar baada ya sakata la muda mrefu dhidi ya TP Mazembe
–
Baada ya Mtibwa kuinasa saini ya Kanda, waliwekewa ngumu na miamba hiyo ya Lubumbashi ambao walidai wana mkataba na Kanda huku mchezaji mwenyewe akikakana
–
Mgogoro huu ulifika mpaka FIFA na sakata limechukua zaidi ya miezi mitatu mpaka kupata ufumbuzi ambapo Mazembe wameshindwa kesi kutokana na kukosa vielelezo sahihi
–
Kwa maana hiyo Kanda sasa ni ruksa kucheza mechi za Mtibwa, lakini pia tayari wamemalizana na Kitayose juu ya kulipa gharama ambazo nao walitoa kipindi wanaisaka saini yake.