Gari la Kifahari la mchezaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo limepata ajali baada ya kugonga nyumba kisiwani Mallorca nchini Hispania.
–
Gari hilo aina ya Bugatti Veyron lenye thamani ya pauni milioni 1.8 lilikuwa likiendeshwa na mfanyakazi wake, nyota huyo na familia yake hawakuwemo kwenye gari.
–
Dereva wa gari ameripotiwa kutoka bila majeraha lakini gari hilo limeharibika sana kwa mbele pia limeharibu vibaya sehemu ya mbele ya nyumba iliyoigonga. Ronaldo pamoja na familia yake wamekuwa kisiwani humo tangu wiki iliyopita kwa mapumziko.
–
Gari hilo ni moja kati ya magari mawili ambayo Ronaldo aliyasafirisha kwenda Mallorca kwa matumizi kipindi cha mapumziko. Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.