Mwanamuziki nguli wa muziki wa bongo fleva Abubakari Katwila maarufu Q Chief ameweka wazi sababu kadhaa za kutokuwa na ukaribu na maelewano mazuri kati yake na msanii Harmonize kama ilivyokuwa hapo awali.
Chilla amemtuhumu msanii huyo kuwa na tabia ya ukabila, na kuitaja sababu hiyo kama chanzo cha msanii Country Wizzy kujiengua na Label ya Konde Music WorldWide.
“Namheshimu Harmo lakini sioni kwamba alinipa ile gari, eti kwamba ilikuwa ni kila kitu kwenye maisha yangu, thats a small car for Q chief, Q chief is a big man for that car.
Nilivyoondoka mimi sikuwa nimesainiwa, lakini Country Boy alikuwa amesainiwa lakini alishindwa kukaa na kuvumilia. Ana ukabila kidogo ambao sio mzuri, ambao Diamond Platnumz hana huo ukabila wala Ali Kiba hana huo ukabila, inabidi autoe.” amesema Q chief
Chilla ameyasema hayo kwenye mahojiano yake na channel E, ambapo alidokeza kushangazwa na kwanini Harmonize hakumjumuisha msanii Country Boy kwenye safari yake ya nchini Marekani na badala yake akamchukua msanii wake Ibraah na kwenda naye kitu ambacho amedai kuwa hakuona umuhimu wake.
@harmonize_tz
@kondegang
@official_qchief