Baada ya msanii maarufu wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ’Harmonize’ kumvalisha pete ya uchumba msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja.
–
Tukio hilo limefanyika jana Jumamosi Juni 25,2022 hoteli ya Serena na kulipa jina la ‘Late Lunch’ huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang, Mkurugenzi wa TVE, Francis Ciza ’Majizo’, Aunty Ezekiel, Martin Kadinda na wengineo.
–
Wawili hao wamechumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu walipotengana baada ya mwanamuziki huyo kumfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu.
–
Kwa upade wake Kajala amesema: “Hakuna asiyejua tuliyoyapitia, pia mimi si mkamilifu so nikaona kwa nini nisimsamehe, So Harmonize naahidi nitakupenda leo, kesho hadi milele,”.