Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeingilia kati na kutimua maandamano na vurugu zilizotokea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde zilizohusisha waumini wa kanisa hilo.
–
Ofisa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Johanes Bitegeko akiwa na askali wengine waliingia maeneo ya kanisa hilo na kuwatawanya waumini waliokuwa wamekusanyika makundi mawili tofauti wanaomuunga mkono Askofu Mwakihaba na Dk Mwaikali.
–
Akizungumza eneo la tukio, Bitegeko amesema mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na kuwataka watu wote kutawanyika akisema bado unashughulikiwa.
–
“Sina mambo mengi, kazi yetu ni kushughulikia usalama, mmekusanyika bila sababu za msingi tunaomba muondoke muendelee na shughuli za uzalishaji” amesema Ofisa hiyo.
Sosce : Mwanachi