
Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, John Pambalu amewaomba wanachama wa chadema kuendelea na mapambano ya kudai Katiba mpya mpaka pale adhima hiyo itakapotimia.
–
Pambalu amesema hayo katika kikao cha majadiliano ya hatima ya Katiba mpya yaliyojumuisha wanachama na viongozi wa chama hicho kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kilichofanyika Mjini Geita.
–
Amesema juhudi za kudai katiba mpya zinapaswa kuwa endelevu kwa wanachama wa Chadema na kwa watanzania wote kwa kuwa mahitaji ya katiba mpya ni ya Taifa na siyo ya kwa ajili ya Chama cha Chadema.
–
Amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeonekana kuunga mkono juhudi za kudai Katiba mpya lakini wao Wana wajibu kuongeza nguvu kukamilisha safari ya mabadiliko.
–
“Tumefikia hatua CCM wanasema Katiba mpya ni sasa lakini sisi bado tataendeleza mapambano kudai Katiba mpya kwetu ni Kama vita” amesema Pambalu.