Rapa maarufu wa Marekani Lil Wayne (39) hataweza kutumbuiza katika tamasha maarufu la ”Strawberries and Creem” hapa Uingereza baada ya mamlaka ya uhamiaji kumnyima viza kutokana na hatia zake za zamani.
–
Waandaaji wa tamasha hilo wamesema kuwa ”Lil Wayne amenyimwa viza ya kuingia Uingereza katika dakika za mwisho. Tumesikitishwa.”
–
Mamlaka husika imesema kuwa ”mtu yoyote ambaye amewahi kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 au zaidi lazima maombi yake yakataliwe.”
–
Mwaka 2010 Wayne ambaye jina lake halisi ni Dwayne Carter alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kutokana na kukutwa na bunduki kinyume na sheria.
–
Mwaka 2019 Wayne alikutwa tena akiwa na bunduki pamoja na risasi kinyume na sheria. Kosa hilo lingeweza kumfunga jela kwa miaka mingi lakini alipewa msamaha na Rais wa Marekani aliyepita Donald Trump katika siku yake ya mwisho madarakani.