
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho watumishi 1,048 wa kubadilisha vituo vya kazi pekee. Watumishi hao ni wale walioomba uhamisho kuanzia Mwezi Februari-Mei, 2022.
–
Aidha amewakumbusha watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa uhamisho wa kwenye Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji umesitishwa mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
–
Amewataka watumishi waliopata uhamisho huu kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kufika Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo.
–
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT