ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, July 2, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Makocha Kutoka Sehemu Mbali Mbali Duniani Wamiminika Kutaka Kibarua Cha Pablo Simba

I am Krantz by I am Krantz
Jun 3, 2022
in HABARI, MAGAZETI TANZANIA
0
PABLO AWATUPIA LAWAMA WACHEZAJI WAKE
0
SHARES
47
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

KLABU ya Simba imesema kuwa imepokea maombi kwa simu na barua pepe kutoka kwa mawakala na makocha mbalimbali duniani wakitaka kibarua cha kuifundisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, baada ya kumtimua kocha wao Pablo Franco.

Pamoja na hayo, klabu hiyo imesema imekuwa ikiingia makubaliano na baadhi ya wachezaji, lakini haijaanza rasmi usajili hadi hapo itakapitia ripoti ilioachwa na kocha aliyepita, lakini na mapendekezo ya kocha mpya atakayekuja.

RelatedPosts

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

Jul 2, 2022

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JULAI 2, 2022

Jul 2, 2022

Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.

Jul 2, 2022
Load More

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema jana tangu ilipoachana na kocha Pablo na kutangaza rasmi Mei 31, imekuwa ikipata maombi kutoka kwa makocha mbalimbali kurithi mikoba yake.

“Kuna wakati kila baada ya saa moja tunapata simu pamoja na barua pepe, lakini tangu kocha aondoke tumepata maombi mengi kutoka kwa mawakala ambao wamekuwa wakituambia wana makocha wazuri, pia makocha wenyewe kutoka pande mbalimbali za dunia wamekuwa wakitupa wasifu wao ili tu kuisaka kazi ya kocha aliyepita.

Kumiminika kwa maombi haya siyo kwamba kuna uhaba wa ajira la hasha, ila ni kwa ajili ya ukubwa na Simba, kila kocha mkubwa na mwenye viwango angependa kuja kuifundisha Simba, lakini hiyo haitufanyi sisi tuingie kwenye presha hizo, tutakaa na kuangalia nani atatufaa.

ADVERTISEMENT

Hata sisi tunafuatilia mpira tunafahamu makocha wazuri, kwa hiyo atakayekidhi vigezo ndiyo atakayekuwa kocha wa Simba na tunawaahidi wanachama na mashabiki wa Simba tutawaletea kocha mwenye viwango vya dunia.” Alisema.

ADVERTISEMENT

Kuhusu usajili alisema harakati za kuingia makubaliano zimeanza, lakini hawajaanza usajili rasmi.

“Usajili hatujaanza rasmi, tumeelekeza jicho kusaka kocha, tukimpata kocha ndani ya wiki hizi mbili, ndiyo tutaanza mipango ya kukaa na kocha kutuambia anataka wachezaji wa aina gani na yeye aone wachezaji waliopo. Mapendekezo ya kocha aliyepita na kocha mpya ndiyo yatatuelekeza na kutupa mwanga na taswira ni aina gani ya wachezaji ambao tunakwenda kuwasajili.” Alisema Ahmed.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI
HABARI

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

by Shabani Rapwi
Jul 2, 2022
NEYMAR KUONDOKA PSG
HABARI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JULAI 2, 2022

by Shabani Rapwi
Jul 2, 2022
Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.
BIASHARA

Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.

by I am Krantz
Jul 2, 2022
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASA KWENYE NYAYA ZA UMEME
HABARI

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASA KWENYE NYAYA ZA UMEME

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022
MTUMISHI WA TANESCO AKUTWA GUEST AMEFARIKI
HABARI

MTUMISHI WA TANESCO AKUTWA GUEST AMEFARIKI

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022
SIKUKUU YA EID EL-ADH’HAA JULAI 10, 2022
HABARI

SIKUKUU YA EID EL-ADH’HAA JULAI 10, 2022

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In