
Dar es Salaam, Alhamisi 16 Juni, 2022
1.0 Utangulizi
Serikali ya awamu ya sita (6) ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania imewasilisha bajeti yake ya taifa kwa mwaka 2022/2023. Kwa maoni yetu, bajeti inaeleza dhamira thabiti ya Serikali ya kuongeza kasi ya kufufua uchumi na kuimarisha sekta ya uzalishaji mali kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania.
Hotuba ya bajeti imeweka wazi nia ya serikali katika kuhakikisha sera nzuri za mapato na matumizi zinazotekeleza thamani ya fedha, mapambano dhidi ya rushwa na uwekezaji katika sekta za uzalishaji mali ili kuongeza ajira kwa vijana jambo ambalo linasisitiza umuhimu wa ufanisi wa Sekta Binafsi kwa ufanisi katika utekelezaji wa kazi hii.
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) linaipongeza Serikali kwa kuwasilisha bajeti yenye uwiano na inapenda kuihakikishia Serikali dhamira yake na msaada wake katika kuwezesha kufikia uchumi ulioimarika kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021-2026 na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na wanachama wake wanapenda kuchukua fursa hii kuipongeza Serikali ya Awamu ya 6 chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk. Mwigulu Nchemba (Mb), na Serikali kwa ujumla kwa bajeti nzuri sana.
2.0 CTI inaipongeza Serikali kwa kufanya mabadiliko mbalimbali katika Muundo wa Kodi, Ada, tozo na marekebisho ya sheria na kanuni ili kuboresha mazingira ya biashara kama ifuatavyo:
Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004
- Kupunguza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye malighafi za kutengeneza taulo za watoto (Baby Diapers)
- Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ambazo zinatambulika kwa HS code 4804.29.00.
- Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 badala ya asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye ngano inayotambulika kwa HS Codes 1001.99.10 na 1001.99.90 kwa utaratibu wa “Duty Remission”
- Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwa utaratibu wa Duty Remission kwenye bidhaa ijulikanayo kama “Printed Alluminium Barrier Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90
- Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kutoka kiwango cha awali cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye malighafi ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD Palm Stearin HS Code 90.40 kwa viwanda vinavyotengeneza sabuni nchini.
- Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA(Organic surface-active agents – Anionic) inayotambulika kwa HS Code 3402.11.00 kwa utaratibu wa Duty Remission.
- Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji wa pikipiki za matairi matatu bila kujumuisha fremu ili ziweze kutengenezwa na kuunganishwa hapa nchini (CKD for three-wheel motorcycles excluding chassis and its components) zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa utaratibu wa Duty Remission.
- Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kutoka kiwango cha asilimia 100 au dola za Marekani 460 kwa kila tani moja ya ujazo (metric tone) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwa mwaka mmoja kwenye sukari ya matumizi ya viwandani.
- Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza sabuni (toilet soap) zinazotambulika kwa HS Code
3401.20.10.
- Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza vioo vizito (toughened glass) zinazotambulika kwa HS Codes 10.00; 7005.21.00; 7005.29.00; na 7005.30.00.
- Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 25 au asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi zinazotumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio aina ya maboksi (corrugated boxes).
- Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza viongeza ladha kwenye vyakula na vinywaji (food flavors) zinazotambulika kwa HS Code 1901.90.10; 3302.10.00; na 3505.10.00.
- Kurejesha utozaji wa Ushuru wa Forodha wa kiwango cha asilimia 0 kutoka kiwango kilichokuwa kinatumika cha asilimia 25 kwenye mafuta ghafi ya kula (Crude Palm Oil) yanayotambulika kwa HS code 1511.10.00.
- Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za Marekani 500 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye mafuta ya kula yaliyochakatwa kwa kiwango cha kati na cha mwisho (semi-refined and refined)
Maoni ya CTI:
Hatua hizi za kikodi zitawezesha wazalishaji wa ndani kupunguza gharama za uzalishaji, kuboresha mahusiano na wateja, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, kuboresha ushindani na kusisimua ukuaji wa uchumi.
- Maeneo yanayohitaji kutazamwa zaidi na Serikali
Tunaposhukuru hatua hizi za Serikali, tungependa kuonesha baadhi ya maeneo ambayo yanaweza kuathirti maendeleo ya ukuaji wa viwanda na tungependekeza serikali kuchukuwa hatua kama ifuatavyo:
- Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za pamba (cotton yarn) zinazotambulika kwa Headings 05, 52.06 na 52.07 isipokuwa nyuzi za pamba zinazotambulika kwa HS Code 5205.23.00.
- Kutoza ushuru wa bidhaa wa shilingi 700 kwa kilo ya bidhaa za sukari (sugar confectionery) zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na shilingi 500 kwa kilo ya bidhaa za sukari zinazozalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 31.00, 1806.32.00, 1806.90.00, (chokoleti), 1905.31 (biskuti) na 1704 (chingamu).
- Kulinda viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa za chuma dhidi ya bidhaa zinazotoka nje, CTI bado inapendekeza kuongeza ushuru wa forodha kutoka 25% au Dola 250 kwa Mita moja ya ujazo hadi 35% au Dola 350 kwa mita moja ya ujazo kutegemea Kiwango kitachokuwa kikubwa.
- Vipaumbele muhimu vya Bajeti kwa maendeleo ya viwanda na ukuwaji wa uchumi katika kipindi cha 2022/2023
Tumefurahi na tungependa kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuzingatia vipaumbele vinavyolenga kuleta ushindani na ustawi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya watu kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Miaka Mitano 2022-2025/26
Sera muhimi za kifedha na vipaumbele vya kukuza viwanda vilivyoainihwa katika bajeti ya mwaka 2022/2023 ni pamoja na:
- Kuongeza na kuimarisha makusanyo ya mapato ya Serikali
- Kupambana na Rushwa
- Kuimarisha matumizi ya mifumo ya tehama katika kukadiria kodi na matumizi ya mfumo wa GePG
- Kutoa elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Kidato cha sita
- Kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kufungua fursa zaidi kwa sekta binafsi kufanya biashara.
· Kuendeleza mpango wa serikali kujenga vituo vya kutolea huduma ya pamoja (One-stop-center) ili kuhakikisha kuwa mahitaji yote ya huduma za kibiashara yanapatikana sehemu moja. · Kupunguza matumizi ya serikali
- Kuongeza bajeti katika sekta ya uzalishaji kama vile Kilimo, Mifugo, Uvuvi n.k ili kuongeza ajira kwa vijana.
- Kuendelea kutoa mikopo katika biashara na sekta mbalimbali za uchumi.
- Kuendelea kuzalisha, kusambaza na kujenga Bwawa la kuzalisha Umeme la Julius Nyerere – 2,115 MW; Ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga -Tanzania na mradi wa kuchakata na kusambaza gasi asilia.
- Ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR, Barabara na Madaraja
- Kuendelea kuboresha bandari ili kukuza shughuli za kiuchumi, kuboresha usafiri wa majini; kukuza uvuvi katika bahari ya kina kirefu
- Kuendelea kuboresha shirika la Ndege la Tanzania
5.0: Bajeti ya 2022/2023
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mjini Dodoma siku ya Jumanne, Waziri wa Fedha na Mipando Dkt. Mwigulu L. Nchemba (MB) alisema kuwa jumla ya 41.48 trilioni zitarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka wa fedha 2022/2023ikilinganihwa na 37.99 trilioni zilizotumika katika mwaka wa fedha 2021/2022, ambalo ni takribani ongezeko la asilimia 9.5.
Jumla ya mapato ya ndani (yakijumlisha ya serikali za mitaa (LGAs) na mapato yake yenyewe) yanatarajia kufikia 28.02 trilioni, sawa na asilimia 67.5 ya bajeti yote.
Serikali inapanga kikusanya kodi inayofikia 23.65 trilioni na mapato yanatokana na vyanzo visivyo vya kodi vinavyotozwa na Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa yanayokadiriwa kufikia 4.37 trilioni.
- Hitimisho:
CTI inaimani kuwa, kama ikitekelezwa vizuri, bajeti ya mwaka 2022/2023 itasaidia kwa kiasi kikubwa juhudi za serikali kujenga uchumi wa viwanda endelevu. Shirikisho la viwanda Tanzanialinaahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na serikali ya awamu ya sita kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ya kijamii na kiuchumi.
CTI Secretariat
P O Box 71783
Dar es Salaam
Tel: 2114954/ 213802/ 2130327
E-mail: cti@cti.co.tz