Baada ya mchambuzi wa kituo cha EFM Radio, Jemedari Saidi kusema kuwa Hersi Said hafai kuwa Rais wa klabu ya Yanga SC kwa kuwa anatoka kwenye kampuni ya GSM, ambaye ndiye muwekezaji katika klabu hiyo.
–
Kauli hiyo imemwibua msemaji wa Yanga, Haji Manara na kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kumwandikia barua ya wazi, Mmiliki wa EFM Radio, Francis Ciza maarufu Majizzo.
–
“Majizzo hii ni barua ya wazi toka kwa msemaji rasmi wa klabu ya Yanga SC. Katika radio unayoimiliki unaye mchambuzi mmoja ambaye Kila kukicha yeye ni kuisema klabu yetu kwa mabaya, aidha atawasema Wachezaji wetu, aidha viongozi wetu au wafadhili wetu na mara kadhaa watendaji wa klabu nikiwemo mimi binafsi”
–
“Ni trend ya mwaka mzima sasa, hufanya hivyo akiwa studio kama alivyofanya hapo juu, au kupitia page zake mtandaoni, na wakati mwingine hata anapohojiwa na vyombo vingine vya habari”
–
“Tumemvumilia vya kutosha bro, tumekuwa na tolerance ya kiwango cha juu na kwa muda mrefu sana, binafsi nilishalilalamikia sana hili jambo kwa mazungumzo na uongozi wako lakini hakuna mabadiliko”
–
“Uvumilivu wetu unakaribia ukomo hivi karibuni,, Yanga haikatai kukosolewa, lakini kuikosoa Taasisi yetu kwa mambo ya uongo na wakati mwingine kwa dhihaka, tena kila wakati toka kwa mtu yuleyule HAIVUMILIKI”
–
“Kwa mfano hiki kitendo cha leo ni KUHARAS uchaguzi wetu wa klabu, ni kutaka kuuvuruga uchaguzi huu, na ni kutaka kuwapangia Wanachama juu ya Taasisi yao”
–
“Tunakupa muda uchunguze madai yetu wewe mwenyewe na uone hii ni sawa kwa Radio yako kutumika na mtu mmoja kuifedhehesha Taasisi nyingine ?!”
–
“EFM Radio inawasikilizaji wengi na wenye itikadi tofauti tofauti za kishabiki, je mngetamani kuona uhusiano wetu wa kikazi na Radio yenu unaisha kisa mtu asiye na maadili na heshma ambaye kutwa nzima ni kusema mabaya tu Yanga ?!”
ADVERTISEMENT